Tusitumie Njia Ya Udanganyifu Kwa Kujipatia Mali

Margaret Kayombo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Masimulizi …

by Margaret Kayombo (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Hapo zamani za kale Abunuasi alikwenda kuazima sufuria kwa jirani yake. Baada ya siku tatu hivi, akairudisha sufuria hiyo pamoja na sufuria nyingine ndogo ndani yake. Jirani akazipokea huku akisema hii ndogo siyo yangu mimi nilikuazima hii kubwa tu. Abunuasi akamjibu, hapana hata hiyo ndogo ni yako, sufuria kubwa ilizaa, hiyo ndogo ndiyo mtoto wake. Jirani alistaajabu sana kusikia kwamba sufuria imezaa. Lakini akafurahi kupata sufuria nyingine. Akamshukuru sana Abunuasi na akamwomba aje kuazima sufuria zake wakati wowote.

Baada ya kama mwezi mmoja hivi, Abunuasi akaenda tena kwa jirani yake. Akamwambia ana karamu na anahitaji kuazima kama sufuria tatu kubwa. Jirani pasipo shaka akampa Abunuasi sufuria harakaharaka kwa tamaa kwamba zitazaa tena. Abunuasi akazichukua akaenda zake. Safari hii, jirani akaona Abunuasi amechelewa kuzirudisha sufuria lakini akajipumbaza kidigo kuwa pengine zimo katika hali ya kuzaa mapacha. Wiki ikapita, wiki mbili, wiki tatu, nne, aah! Sufuria hazijarudishwa. Jirani akaona afadhali aende akaulize. Alipofika kwa Abunuasi akauliza habari ya sufuria zake. Akaambiwa kwamba sufuria zake zote zimefariki katika hali ya kijifungua, pamoja na watoto wao na kwamba yeye amekwishazizika na kuzifanyia matanga. Jirani aliposikia hivi, hasira zikampanda. Akamwita Abunuasi ni mwongo na mwizi, akidai kwamba ni udanganyifu. Akasema kwa sauti na hasira, “Iinawezekanaje kitu kama sufuria ambacho hakina uhai kufariki dunia, kuzikwa na kufanyiwa matanga”?Abunuasi akamjibu: “Jirani yangu, kumbuka kwamba kila kizaacho hakina budi kufa.

Katika hii simulizi kuna mafundisho kadhaa.

  1. Tusiwe waongo maana uwongo unasababisha kumkosesha mtu au watu kukosa haki yake/ yao.
  2. Kuwa mtu mwongo katika jamii ni kitu kibaya sana, hata ikatokea kama ukisema jambo la kweli jamii itaelewa kuwa unasema uwongo.
  3. Uwongo unakufanya mtu kuwa mwenye sifa mbaya kwako mwenyewe na hata mpaka kwenye familia yako.
  4. Daima mtu mwongo hupata vitu au mali kwa njia ya utapeli na wizi.
  5. Ukiwa mwongo maisha yako ni ya mashaka na ya kukosa amani.
  6. Yatupasa tujipatie mali au vitu kwa njia ya uhalali siyo kutumia elimu ya uwongo au mazingaombwe.
  7. Tuwe wa kweli kwa jamii tunayoishi nayo. Ukikopa, rudisha au kama huna muda huo ongea ukweli ili jirani ajue na hata ukiazima kitu cha jirani yatupasa kurudisha kwa wakati siyo kuleta Kiswahili kirefu na kejeli kama za Abunuasi.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Published by Wisdom&Wellness

MENTAL HEALTH & WELLNESS Tap Elderly Women’s Wisdom for Youth (TEWWY) is a mental health stakeholder in Tanzania bridging the intergenerational- and mental health treatment-gap by training retired elderly women in adapting WHO’s mental health Gap Action Program (mhGAP). The grandmotherly figures called Wisdom&Wellness Counselors provide accessible mental health services, support and resources in their underserved communities. Wisdom&Wellness Meditation Garden is a wellness center in the Washington DC Metropolitan Area empowering people with simple self-care practices for holistic health and well-being. We teach yoga; organize nature adventures in local parks; facilitate Wisdom&Wellness Talks, a safe-space for people to share wisdom, connect, gain life-skills as they build community; and the Wisdom&Wellness Collection, our handcrafted line of natural skincare & aromatherapy products. 50% of our Wisdom&Wellness Meditation Garden’s revenue supports the mental health initiatives of our nonprofit partner in Tanzania, TEWWY If you would like to be a part of our Wisdom&Wellness Community, let’s connect.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: