Tuwashirikishe Watoto Kazi Za Shamba Kwa Mafanikio

Grace Mshanga - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Masimulizi …

by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Zamani kidogo alikuwepo baba mmoja aliyeitwa Minja, kwa sasa ni marehemu. Alikuwa ni mmiliki halali wa mabasi manne ya usafirishaji ya kutoka Moshi kwenda Singida. Minja alikuwa na tabia ya kujinyima sana, pamoja na kuwa na wafanyakazi wengi yeye mwenyewe alipenda sana kilimo, alikua na gari aina ya Landrover ambalo alikuwa anaenda nalo shambani kila siku, umbali wa  kilomita kama 30 hivi toka nyumbani kwake. Alikuwa akiondoka kwenda shamba asubuhi na mapema saa 11 alfajiri na kurudi saa 11 au 12 jioni.

Cha kushangaza chakula alichobeba cha kuliwa mchana kutwa ni mahindi ya kuchemshwa yaliotiwa chumvi tu na maji ya kunywa , wakati mwingine ndizi za kuchoma na chai ya rangi au viazi vikuu vya kuchoma na chai ya rangi. Hivyo ndivyo vilikuwa vyakula vyake akibadilishabadilsha siku zote aendapo shamba. Mafanikio katika kilimo na magari yalikuwa makubwa sana aliweza kuongeza magari ya  usafirishaji yakafika sita. Aliendelea kwenda shamba na aina ya chakula kilekile hadi utu uzima sana na baadaye kufariki. Watoto wake waliweza kurithi mali nyingi alizoziacha kwa raha mstarehe. Mara nyingi mali ya kurithi haina uchungu. Aliyepata uchungu kuitafuta anakufa bila kunufaika nayo.

Hapa tunajifunza mambo mengi. 
1. Hapa duniani tunapita, tufanye kazi kwa bidii lakini pia tuangalie afya zetu. 
2. Tusijinyanyapae kwa kujinyima lishe bora eti kwa kisingizio cha kuweka akiba.  Tufanyapo kazi nzito tule mlo kamili ili kujenga afya zetu. 
3. Tutafute wasaidizi na kuwalipa ujira. Kwa kufanya hivyo tutakuwa pia tunawasaidia wenye shida ya kipato na hapo hapo tutakuwa tunapumzika kutokana na kazi nzito.  Kwa utajiri aliokuwa nao Minja angetumia sehemu ndogo tu kuweka vibarua kumsaidia shambani. 
4. Kushirikisha watoto wetu kwenye kazi mbali mbali pamoja na kilimo kwa ajili ya maendeleo ya familia. Wazazi wasibebe kazi zote peke yao .
5. Maisha ni mafupi sana, yatupasa kuwa na mpangilio mzuri ili kukwepa suluba zinazoweza kutupata kutokana na kujinyima kupindukia. 

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Published by Wisdom&Wellness

MENTAL HEALTH & WELLNESS Tap Elderly Women’s Wisdom for Youth (TEWWY) is a mental health stakeholder in Tanzania bridging the intergenerational- and mental health treatment-gap by training retired elderly women in adapting WHO’s mental health Gap Action Program (mhGAP). The grandmotherly figures called Wisdom&Wellness Counselors provide accessible mental health services, support and resources in their underserved communities. Wisdom&Wellness Meditation Garden is a wellness center in the Washington DC Metropolitan Area empowering people with simple self-care practices for holistic health and well-being. We teach yoga; organize nature adventures in local parks; facilitate Wisdom&Wellness Talks, a safe-space for people to share wisdom, connect, gain life-skills as they build community; and the Wisdom&Wellness Collection, our handcrafted line of natural skincare & aromatherapy products. 50% of our Wisdom&Wellness Meditation Garden’s revenue supports the mental health initiatives of our nonprofit partner in Tanzania, TEWWY If you would like to be a part of our Wisdom&Wellness Community, let’s connect.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: