Tuthamini Nyumbani Tulipotoka

Victoria Nakajumo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Masimulizi …

by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Kuna baba mmoja alikuwa na nafasi nzuri sana kazini na maisha yake yalikuwa mazuri. Watoto wake walikuwa wanasoma shule za kulipia tena ada kubwa. Mke wake alikuwa mfanya biashara anafuata bidhaa China na Thailand. Huyu baba kwao ilikuwa ni Tanga kijiji cha Hale. Kwa kweli ilikuwa ni familia iliyokuwa inaishi maisha ya kifahari hata nyumba waliyokuwa wanaishi ilikuwa ni nzuri sana. Magari walikuwa nayo, mke alikuwa na la kwake na mume hali kadhalika. Watu walikuwa wanawatamani jinsi walivyokuwa wakiishi.

Katika maisha kila mtu hupitia magonjwa. Baba alianza kuugua, lakini kwa vile wana uwezo aliweza kumudu matibabu mazuri na ya gharama kubwa bila matatizo. Marafiki zake pia walikuwa na uwezo hivyo waliweza kumsaidia katika matibabu.

Pamoja na yote, hali iliendelea kuwa mbaya, mwisho yule baba alifariki dunia. Wanandugu waliamua kuuchukua mwili na kupeleka Hale walikokuwa wazazi wake kwa mazishi.
Taratibu zote zilifanywa, mwili ukasafirishwa kwenda Hale. Cha kushangaza, walipofika Hale kulikuwa hakuna nyumba inayofanana na hadhi yake marehemu, na wala kwa wazazi hapakuwa pazuri, kwani nyumba ilikuwa ni ya miti. Ilikuwa ni aibu tupu kwa majirani na marafiki waliokuwa wamemsindikiza swahiba wao.

Mazungumzo baina ya wasindikizaji yalikuwa ni ya kumsema marehemu kuwa alikuwa hajali kujenga kwao. Walimdharau kimya kimya na baada ya mazishi waliondoka kurudi makwao.

Hili ni somo kwa kila mtu. Ni muhimu kujenga nyumbani ulikotoka na pia kuwajengea wazazi wako nyumba nzuri ili kuepuka aibu kama ilivyotokea kwa huyu bwana ambaye mjini alikuwa na maisha ya juu lakini kijijini kwake ni aibu tupu.

Yatupasa kukumbuka na kuwekeza nyumbani tulikotoka.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Published by Wisdom&Wellness

MENTAL HEALTH & WELLNESS Tap Elderly Women’s Wisdom for Youth (TEWWY) is a mental health stakeholder in Tanzania bridging the intergenerational- and mental health treatment-gap by training retired elderly women in adapting WHO’s mental health Gap Action Program (mhGAP). The grandmotherly figures called Wisdom&Wellness Counselors provide accessible mental health services, support and resources in their underserved communities. Wisdom&Wellness Meditation Garden is a wellness center in the Washington DC Metropolitan Area empowering people with simple self-care practices for holistic health and well-being. We teach yoga; organize nature adventures in local parks; facilitate Wisdom&Wellness Talks, a safe-space for people to share wisdom, connect, gain life-skills as they build community; and the Wisdom&Wellness Collection, our handcrafted line of natural skincare & aromatherapy products. 50% of our Wisdom&Wellness Meditation Garden’s revenue supports the mental health initiatives of our nonprofit partner in Tanzania, TEWWY If you would like to be a part of our Wisdom&Wellness Community, let’s connect.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: