BUSARA ZIANGUKIAZO KWENYE “T” TATU

Sixtha Komba – Monitoring & Evaluation Officer, TEWWY

Mama Sixtha Komba anatueleza juu ya T tatu ambazo unaweza tumia katika kuyakabili matatizo ukutananayo. Akianza na fafanuzi juu ya T tatu.

  • T1 ni Tatizo
  • T2 ni Tatuzi
  • T3 ni Tokeo

Mama Sixtha Komba anaendelea kufafanua hizi T tatu katika nyanja mbili, hasi na chanya kwa kutumia mfano wa mwanafunzi aliyefeli mitihani yake na jinsi wazazi wanavyolipokea swala hilo.

Matumizi hasi ya T tatu

T1 ambayo ni Tatizo – Kijana kafeli mtihani

T2  ambayo ni Tatuzi – Wazazi/walezi wanamkasirikia na kuamua kumfukuza nyumbani

T3  ambayo ni Tokeo – Kijana anaingia mtaani na kujiingiza kwenye makundi mabaya kama uvutaji bangi, wizi, unywaji wa pombe kupita kiasi au kuamua kujidhuru.

Matumizi chanya ya T tatu

T1  ambayo ni Tatizo – Kijana kafeli mtihani

T2 ambayo ni Tatuzi – Wazazi/walezi wanaamua kumtia moyo kijana wao na kutaka kujua kwanini alifanya vibaya ili wamsaidie.

T3  ambayo ni Tokeo – Kijana baada ya kutiwa moyo na wazazi/walezi anaamua kurudi shule akiamini atafanya vizuri na atakuwa msaada katika jamii, kwani mti mmoja hauanguki mara mbili.

Contact Us

Don’t hesitate to reach out with the contact information below, or send a message using the form.

Tap Elderly Women’s Wisdom for Youth

Tewwy, Jemedali St, Dar es Salaam, Tanzania

+255 737 773 982 | +255 757 327 878 tewwy@tewwy.org

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: