Magreth KayomboWisdom&Wellness Counselor Kibo, Dar-es-Salaam Moyo huficha siri nyingi, nzuri na mbaya. Ni vigumu kwa mtu kuelewa undani wa mtu mwingine.
Monthly Archives: March 2021
USIIGE KUNYA KWA TEMBO UTAPASUKA MSAMBA
Magreth KayomboWisdom&Wellness Counselor Kibo, Dar-es-Salaam Msemo huu ni onyo kwa wanaopenda kuiga bila kufikiri.
UZURI WA MKAKASI NDANI NI KIPANDE CHA MTI
Magreth KayomboWisdom&Wellness Counselor Kibo, Dar-es-Salaam Usiwe mwepesi kudanganywa na unachokiona nje, ndani kinaweza kisiwe kizuri. Ni vema kuchukua muda na kukichunguza kwa kina ili kujiridhisha.
KUVUJA KWA PAKACHA NAFUU KWA MCHUKUZI
Magreth KayomboWisdom&Wellness Counselor Kibo, Dar-es-Salaam Kususia jambo linalohusu jamii au hata mtu mwingine kwa sababu ya tatizo binafsi kunaleta unafuu kwa wale wanaobakia. Kwa upande mwingine inaweza kuwa ni maneno ya kujifariji wewe mwenyewe baada ya watu kukususa.
MTU MWENYE AIBU HUFIA UPENUNI MWA NYUMBA
Paulina NgwawasyaWisdom&Wellness Supervisor Ilala & Kinondoni, Dar-es-Salaam Ni vema kushirikisha watu matatizo yanayokusibu ili upate msaada na usifikie pabaya.
USITUKANE WAKUNGA NA UZAZI UNGALIPO
Margareth KayomboWisdom&Wellness Counselor Kibo, Dar-es-Salaam Hutumika kama onyo kwa mtu anae dharau huduma muhimu anayopewa, kwani siku nyingine ataihitaji tena. Usemi huu unaweza kufananishwa na ule usemao “Baniani mbaya kiatu chake dawa.”