Sakina BushiriWisdom&Wellness Counselor Pugu, Dar-es-Salaam Hii hutumika kuhimiza watu kufanya kazi kwani kwa kufanya hivyo hutolala njaa. Katika mfano huu, mvuvi hali chakula bila mboga.
Monthly Archives: January 2021
UKIPENDA BOGA, UPENDE NA MAUA YAKE
Christina MandeWisdom&Wellness Counselor Kizinga, Dar-es-Salaam Ukimpenda mtu mpende na makandokando yake. Ina maana kuwa unapompenda mtu uwe tayari kupenda mazuri yake pamoja na yale ambayo hayakupendezi. Hali kadhalika, wapende ndugu zake na wa wale wote anaohusiana nao, usibague.
HAKUNA NJIA NDEFU ISIYO NA MWISHO
Grace MshangaWisdom&Wellness Supervisor Temeke & Ubungo,Dar-es-Salaam Hii huwafundisha na kuwaweka tayari wanandoa wapya kuwa hata tatizo liwe kubwa na limedumu kwa muda kiasi gani, mwisho wake ni kusamehana na kuishi kwa furaha na amani kama mwanzo.
UNAPOFANYA KAZI NI ADHA TU, MAVUNO YAKIWA TAYARI NI VICHEKO
Grace MshangaWisdom&Wellness Supervisor Temeke & Ubungo,Dar-es-Salaam Katika hali ya kawaida binadamu kufanya kazi ni adha lakini mapato yapatikanapo ni kicheko. Hivyo vijana na wana ndoa wapya huhamasishwa kufanya kazi kwa bidii ili kupata mavuno bora na mengi ili kujitunza wenyewe na familia zao.
KIDOLE KIMOJA HAKIVUNJI CHAWA
Paulina NgwawasyaWisdom&Wellness Supervisor Ilala & Kinondoni, Dar-es-Salaam Mwanadamu peke yako huwezi kufanikisha malengo yako katika maisha kwa kujitenga, unahitaji ushirikiano. Pia ina maana kwamba ushirikiano katika jamii ni muhimu sana kwani ushirikiano huleta maendeleo na mafanikio mazuri katika jamii au kazi. Msemo huu unatukumbusha kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa.
ASIYESIKIA LA MKUU HUVUNJIKA GUU
Sakina BushiriWisdom&Wellness Counselor Mangaya, Dar-es-Salaam Usemi huu hutumika kuwaasa watu wasiopenda kufuata/kusikiliza wanayoambiwa na wakubwa; kwani mwishowe hufikwa na matatizo wakajuta.
UKIMTAJA CHUI FUNGA MLANGO
Morris LekuleDirector of Programs & Sustainability Sio tu chui hii ina maana kwamba ukihisi akili yako inahisi hatari fanya jambo la kujihadhari.
KABLA HUJADANGANYWA NA WENZIO HUJAFA
Morris LekuleDirector of Programs & Sustainability Ni mara nyingi unapodanganywa na mwenzio, marafiki au rika kwa kupotezana – sasa usipokuwa na akili ni rahisi kutumbukia kwenye shida. Hivyo basi kama utapokea ushauri unatakiwa kutumia na akili yako pia.
MWENYE KISU KIKALI NDIO MLA NYAMA ILIYONONA
Christina MandeWisdom&Wellness Counselor Temeke, Dar-es-Salaam Mtu akifanya kazi kwa bidii ndiye anaye fanikiwa. Kwa mfano mwanafunzi akisoma kwa bidii ndiye anayefaulu vizuri au mkulima akilima kwa bidii ndiye anayepata mavuno mazuri.
MTEMBEZI HULA MIGUU YAKE
Suzan NjanaWisdom&Wellness Counselor Kigamboni, Dar-es-Salaam Mtu mvivu mara nyingi ni mtembezi na anapenda kuishi kutegemea utembezi wake kula chakula atakachobahatika katika matembezi yake.Huyu ni mvivu,hana kazi maalumu na mtegemezi. Ndugu na jamii inayomjua humwita mtembezi hivyo hula miguu yake kwa kubahatisha chakula njiani kwa watu wanaomsaidia Watu wa aina hii wanaweza kubadilika tabia ya uvivuContinue reading “MTEMBEZI HULA MIGUU YAKE”