BAADA YA JUA KUZAMA, UNAPOANGALIA NA HUWEZI KUMTAMBUA MTU, WASICHANA HAWARUHUSIWI KUTOKA NYUMBANI KWAO
Monthly Archives: January 2021
USIPOZIBA UFA UTAJENGA UKUTA
Sakina BushiriWisdom&Wellness Counselor Mangaya, Dar-es-Salaam Usemi huu hutumika kuhimiza au kuwafunza watu kurekebisha mambo kabla hayajaharibika kabisa. Kwa mfano, nguo ikitatuka kidogo shona usiiache ichanike yote utakuja kushindwa kuirekebisha. Kwa hapa ilivyotumika ukuta ukiwa na ufa uzibe la sivyo utaanguka na kukubidi ujenge ukuta mzima.
UKISIKIA YOWE KIMBIA KUOKOA JAHAZI
Grace MshangaWisdom&Wellness Supervisor Temeke & Ubungo, Dar-es-Salaam Usikiapo yowe lazima kwenda kutatua tatizo. Kuna sauti maalumu hupigwa ikiashiria tatizo limetokea katika jamii au sehemu hiyo, ni lazima kwenda na kumaliza tatizo kwa ushirikiano.
POMBE SIYO MAJI
Grace MshangaWisdom&Wellness Supervisor Temeke & Ubungo Dar-es-Salaam Msemo huu unawaasa watu hasa vijana wasijiinigize kwenye tabia ya kunywa pombe kwa sababu ya athari zitokanazo na matumizi ya pombe.
MTAKA YOTE KWA PUPA HUKOSA YOTE
Sakina BushiriWisdom&Wellness Counselor Mangaya, Dar-es-Salaam Usemi huu hutumika kuwakanya watu wasiokuwa na misimamo thabiti, wenye tamaa, ambao wanapenda kushiriki katika kila jambo litokealo kwa wakati moja. Wasipokuwa waangalifu, tabia hii inaweza ikawafanya washindwe kufanikiwa hata jambo/shughuli moja.
NDEGE MOJA MKONONI NI WA THAMANI KULIKO KUMI WALIO PORINI
Rustica TembeleFounder & CEO Maana yake ni kidogo chochote ulicho nacho ni cha thamani kuliko vingi ambavyo haviko mikononi mwako. Msemo huu unaweza kutumika kwa kuwaasa watu wenye tabia ya kudharau kidogo walichonacho na kushabikia/kutamani kikubwa wasichokuwa nacho..
NJIA YA MUONGO FUPI
Grace MshangaWisdom&Wellness Supervisor Temeke & Ubungo, Dar-es-Salaam Msemo huu una maana kuwa muongo huweza kugundulika kwa urahisi. Usemi huu unatumika kuwajulisha wasema uongo kuwa hugundulika kwa wepesi sana, ukimuuliza maswali mawili matatu unagundua uongo wake hivyo huwahamasisha kusema ukweli.
MTAKA NYINGI NASAHA, HUMKUTA MINGI MISIBA
Sakina BushiriWisdom&Wellness Counselor Mangaya, Dar-es-Salaam Hii hutumika kuwaasa wale wanaopenda kufanya urafiki na kila mtu au kuwafanya kama ndugu zao hukutwa na misiba mingi kwani kila tatizo la mmoja wao litamhusu yeye pia. Msemo huu unaweza kutumika kwa watu ambao wanapenda kujionyesha ni maarufu na hivyo kutaka waonekane wanashiriki kila jambo litokealo, ukweli ni kwambaContinue reading “MTAKA NYINGI NASAHA, HUMKUTA MINGI MISIBA”
NDEGE MJANJA HUNASA KWENYE TUNDU BOVU
Rustica TembeleFounder & CEO Inaweza kuwa na maana ya mtu kufikishwa pabaya pale anapofanya uchaguzi uliopitiliza wa kitu chochote na hatimaye kupata kitu kisicho kizuri. Mathalani, mwanaume anayechagua sana mke au mwanamke anayechagua sana mume anaweza kuishia kupata mke/mume asiyefaa. Usemi huu unaweza kutumika kwa kuwaasa watu wanaofanya chaguzi zilizopita kiasi kwenye maisha.
KWA MUOGA HUWA HAKUNA KILIO
Morris LekuleDirector of Programs & Sustainability Tap Elderly Women’s Wisdom for Youth Wale wanajifanya ni shujaa mbele ya hatari ndiyo wanaopata matatizo mfano kufa, kujeruhiwa.