NJIA NDEFU HUTUPA MAISHA MAREFU

Caroline SwaiWisdom&Wellness Supervisor Kigamboni,Kinondoni & Ubungo, Dar-es-Salaam Tunapotaka kufanya jambo lolote tuwe na subira, tusiharakishe kwani haraka haina baraka. Tunapovuta subira tunapata muda wa kutafakari na kufanya kwa umakini na hatima yake ni mafanikio mazuri.

JITAHIDI KUWA NA MARAFIKI WAZURI WENGI LAKINI AMINI WACHACHE WANAOKUFAA

Christina MandeWisdom&Wellness Counselor Kizinga, Dar-es-Salaam Marafiki wazuri watakuunga mkono kwa mambo yote mema unayofanya au unayofikiri kufanya na pia kutokushabikia kufanya maovu. Hawatasita kukuambia ukweli pale utakapofanya au kufikiria kufanya maovu na daima watakuelekeza njia inayofaa.