Maisha Ni Kama Kuendesha Baiskeli, Usipokanyaga Pedeli Utaanguka

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Maisha yanafananishwa na muendesha baiskeli. Maisha yanaendeshwa na nguvu zako mwenyewe, hakuna mafuta yanayotumika. Hivyo nguvu zako ndio mafuta yenyewe. 

Utashi na akili ya mtu ndivyo vinavyoendesha maisha. Unatakiwa kufikiri sana, kuhangaika hapa na pale ndio uweze kupata majibu ya maisha yako. Na ukipata hayo majibu, hutakiwi kujibweteka, bali unapaswa kusonga mbele huku ukiangalia yajayo. 

Usicheze na maisha, yanaweza kukugharimu na yanaweza kukutoa kwenye reli. Ukishatolewa kwenye reli, kuja kukaa sawa tena itakuchukua muda. Endapo utatoka nje ya reli, unaweza ukakata tamaa kwani kurudi kwake na kuwa ndani ya reli itakuwa changamoto.

Yakupasa uangalie mipango yako. Hakikisha hauingiliwi na mtu ama kuyumbishwa na watu watakaokurudisha nyuma. Daima kumbuka kuwa, muendeshaji wa maisha yako ni wewe mwenyewe, sawa na ambavyo baiskeli huendeshwa na mtu mmoja na si vinginevyo. Ishi kwa akili huku ukijua malengo yako ni yepi hapa duniani. Shikilia barabara usukani, usikubali kuyumbishwa.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

“Malezi Ruksa” Yana Athari Kwa Watoto

Caroline Swai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Malezi Ruksa (Permissive Parenting) ni aina mojawapo ya malezi ambayo mtoto anapewa ruksa ya kufanya au kuchagua chochote anachopenda/anachotaka bila ya kudhibitiwa. Malezi haya humpa mtoto uhuru uliopitiliza kiasi kwamba mtoto anasahau wajibu wake. Hata hivyo, hii ni aina ya malezi inayomfanya mzazi ajione anampenda sana mtoto wake.

Continue reading ““Malezi Ruksa” Yana Athari Kwa Watoto”

Huwezi Kusukuma Gari Bovu Ukiwa Umekaa Ndani Yake

Joyce Msai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Joyce Msai (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Gari ni aina ya chombo cha usafiri kinachoendeshwa kwa kutumia nishati ya mafuta na gesi. Dereva ndiye analiendesha na kulitunza gari. Endapo likipata hitilafu yeyote ile, dereva ndiye atakayelazimika kuteremka chini na kulikagua. Pale atakapogundua kama kuna hitilafu yoyote, ni wajibu wa dereva kutafuta mafundi wa kutatua tatizo hilo kwa kuwa wanayo maarifa ya kutosha.

Katika maisha yetu kuna changamoto mbalimbali zinazotokea na kusababisha majeraha makubwa ya moyo. Matatizo haya yanaweza kuwa ni mtaji mdogo katika biashara, malezi mabaya, umaskini na mengineyo. Mambo haya yanapotokea, yanabaki kuwa mzigo mkubwa moyoni. Jambo zuri la kufanya ni kuwashirikisha watu wengine wenye maarifa zaidi waweze kusaidia katika uratuzi.

Kuna watu waliobeba hazina kubwa, ukiwatumia vizuri watakushauri vizuri kwani wamesheheni busara nyingi na za kutosha. Ukichota busara zao utaweza kutatatua matatizo na kupata mafanikio. Tujifunze kutumia raslimali zilizopo ili tuweze kusukuma magari yetu mabovu. Raslimali zilizopo, ni watu wazima wenye busara za kugawa kwa wahitaji.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection 

Kuishi Kwingi Kuona Mengi

Grace Mshanga - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Kuishi ni neno linalotokana na maisha. Maisha ni siku au miaka tunayojaliwa na Muumba wetu baada ya kuzaliwa. Wenzetu wa zamani waliishi miaka mingi sana, wengine miaka 700 mpaka 900. Nyakati hizi tulizo nazo kuishi kwingi ni miaka 100 tu tena ni kwa wachache sana. Kuishi kwingi na kuona mengi hapa anazungumziwa mtu aliyeishi miaka 50 au 60.

Kuna kisa kimoja kinachomhusu baba mmoja ambaye ameona mengi katika maisha yake. Baba huyu alizaliwa katika familia ya kawaida. Alisoma katika shule zilizojulikana kama middle schools wakati huo. Akiwa shuleni, alikutana na watoto wenziwe wenye tabia za ajabu ambazo hakutarajia kuziona kwa watoto wa ngazi ile. Alipofaulu, alikwenda sekondari. Huko alikutana na wavulana vijana wenye tabia mbali mbali, wengine wavuta bangi na wengine ni kukimbizana na wasichana tu, hata masomo hawazingatii, kwani hawana muda kabisa.

Walikuwepo wale ambao walipenda kujionyesha kuwa wao ni watoto wa matajiri, watoto wa matawi ya juu. Kulikuwepo pia na kundi waliojiita makabwela. Kundi hili lilizingatia masomo, tofauti na kundi la watoto tajiri. Baba huyu alipofika chuo kikuu, aliyaona mambo mengi yakiwa ni ya ovyo ovyo tu, ovyo kuliko yale ya shule za sekondari. Kila mtu alikuwa kivyake vyake na uhuru kibao.

Mzee huyu lakini alikazana na kile kilichokua kimempeleka pale. Alikuwa na lengo la kutimiza matamanio yake. Baada ya kumaliza digrii ya kwanza na ya pili alienda Marekani kwa ajili ya digrii ya uzamivu. Aliyoyaona huko yalikuwa ni zaidi ya yale aliyoyashangaa ya hapa nchini. Alipohitimu digri yake alirejea nchini. Aliitumia elimu yake kuwasaidia Watanzania kwenye masuala ya kuleta maendeleo.

Simulizi hii inatuonyesha kuwa uwapo na umri mkubwa unakuwa umepitia mengi, mazuri au mabaya. Kinachotakiwa ni kuonyesha msimamo wako wa maisha. Hatutakiwi kuiga mambo ya watu wengine, kwani mengine huwa siyo mazuri. Maisha ni kuchagua na kutofautisha kati ya mazuri na mabaya. Huyu mzee alifanya uchaguzi mzuri. Jambo la msingi kwetu sote, tukijaliwa kuishi miaka mingi, yatupasa kufanya uchaguzi mzuri wa maisha yetu.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Mafanikio Makubwa Yana Vikwazo

Victoria Nakajumo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Njia nyepesi kabisa ya kutofika popote ni kusubiri ueleweke na kusifiwa na kila mtu kwa jambo uliloamua kulifanya. Uhalisia ni kwamba huwezi kueleweka kwa kila mtu na sio rahisi sana kusifiwa na kila mtu hasa jambo linapokuwa katika wazo ama hatua za awali.

Ukiwa na jambo unaloliamini, wewe anza; wasiokuelewa sasa watakuelewa huko mbeleni, ila fahamu tu kuwa utakapofanikiwa, kila mtu atakusifu hata waliokupinga na pia wale ambao hawakukuelewa watajifanya walikuelewa na hawatakuwa na namna zaidi ya kukusifu. 

Mafanikio ya mambo makubwa na ya thamani yamo katikati ya miiba ya vikwazo, kupingwa na kudharauliwa. Hapa tunajifunza kitu kimoja. Katika maisha, unapoanzisha jambo lako, Uwe tayari kupata vikwazo ama upinzani mkubwa. Kuna wale ambao watakupa moyo na wengine, watafanya kinyume chake. Yote haya yanaweza kuchangia katika kuvuruga mambo yako na hali kadhalika kuuvunja moyo wako. 

Cha msingi, wewe endelea tu na jambo lako maana mara nyingi baadhi ya watu hawapendi mafanikio ya wengine. Binadamu hatabiriki, leo yuko hivi, kesho yuko vile. Ndio maana, wahenga walinena, binadamu kiumbe mzito, ni vigumu kuyajua yale yaliyojificha moyoni mwake.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection 

Fuata Maadili Uishi Kwa Amani

Avelina Hokororo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Avelina Hokororo (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Amani ni kitu cha msingi sana katika maisha. Unaweza kuwa na kila kitu katika maisha yako lakini ukikosa amani moyoni mwako, yote yanakuwa ni kazi bure. 

Continue reading “Fuata Maadili Uishi Kwa Amani”

Tuwapende Ama Tuwachukie Watu Kwa Kadri

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Kupendana ni jambo la heri na la kupendeza sana.Hata maandiko yanatuasa tupendane. Lakini inabidi tuwe makini katika hilo maana huyo huyo umpendae anaweza kukugeuka siku yoyote. Hapo unaweza hata kujutia ulichokuwa umemfanyia huko nyuma. Uzoefu pia unaonyesha kuwa unaweza ukamchukia sana mtu lakini baadaye akaja kuwa wa msaada sana kwako siku ukipata shida. 

Kuna kisa kimoja kilinitokea nikiwa chuoni. Kuna Mkufunzi mmoja wa hapo chuoni alikuwa hanipendi kabisa. Chuki yake ilikuwa ni ya dhahiri kabisa iliyokuwa ikilenga kunikamata kwenye somo lake ili anifelishe. Kwa bahati mbaya kwake, lakini bahati nzuri kwangu, alishindwa kutekeleza azma yake. Kimasomo, nilikuwa najiweza, lakini ilipokuja katika kutoa maksi, alionekana kuninyima stahiki yangu. Pamoja na yote hayo, sikuwahi kumfuata na kumlalamikia kwa vile anavyonifanyia. 

Tulimaliza mafunzo pale chuoni, tukarudi majumbani na hatimaye kazini. Mimi nilipangiwa kwenda wizarani. Wakati nikiwa pale wizarani, yule Mkufunzi aliyekuwa akinichukia, alikuja pale wizarani. Alikuwa anatafuta jalada lake. Kwa siku mbili nzima, jalida lilikuwa halijapatikana. Kwa bahati tu, nilikutana naye kwenye korido. Nilimchangamkia tu kama vile hakijawahi kutokea kitu chochote baina yetu. Alinieleza shida yake. Kwa moyo mkunjufu, nilienda naye masijala. Tulipofika pale, nilimuomba mtu wa masijala ambaye alitusaidia mara moja. Ndani ya dakika kumi jalada lilipatikana. Mkufunzi wangu aliondoka kuendelea na shughuli zake. Hata hivyo, kabla ya kuondoka alikuja ofisini kwangu kunishukuru kwa yale niliyomsaidia. Baada ya hapo, maisha yakaendelea kama kawaida.

Lakini cha kushangaza pale wizarani kilitokea. Jamaa niliyekuwa nimemuomba anisaidie kupata lile jalada la mkufunzi, alinilaumu sana kwa kumuombea msaada yule Mkufunzi. Bila kumung’unya maneno alisema kuwa yule mkufunzi huwa ana jeuri sana na ndio maana walimsotesha kwa masaa pale masjala. Kwa upole, nilimwambia kuwa yule anayemsema ni Mkufunzi wangu. Nilimuomba amsamehe kwani binadamu hatufanani. 

Tunajifunza kuwa, kama binadamu hatutakiwi kuwa na chuki kwani hatujui mambo yatakayotokea kesho. Yatupasa kupendana na kusaidiana wakati wote. Hata kama tumekoseana, kusameheana ni wajibu. Tusiweke vinyongo mioyoni mwetu. Endapo nami ningelikuwa na kinyongo na yule Mkufunzi, nisingeliweza kumsaidia. Safari yetu ni fupi sana hapa duniani. Tuyafanye maisha kuwa rahisi kuyaishi na si vinginevyo.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Duniani Kuna Watu Waliondaliwa Maisha Na Wanaojiandalia Maisha

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Msemo huu unazungumzia uhalisia wa maisha katika dunia hii tunayoishi. Wako watu wanaishi kutokana na hali ya wale waliowatangulia. Kama wazazi au walezi walikuwa na jina la kusifika, basi kizazi kinachofuata kitatembea katika hali ile ile. Kwa mantiki hii, watakuwa wepesi kuonekana katika eneo lolote lile kutokana na majina makubwa wanayotembea nayo. Mfano kwenye siasa watoto wa wenye majina ni rahisi kufikiriwa na kupata kile wanachokitaka, pamoja na kazi nzuri, kisa tu, jina kubwa linawalinda. 

Anayejiandalia maisha, hata kama ana uwezo inabidi apambane ili aweze kuonekana. Hali kadhalika, inambidi awe na mtu atakayeweza kumtetea. Anaweza akawa mtu waliyefanya naye kazi mahali fulani. Lakini hata kama walifanya kazi pamoja, utendaji wake wa kazi itabidi uwe ulikuwa wa kutukuka sana. Yaani itabidi akumbukwe kwa kazi nzuri alizokuwa akizifanya. Hapo ndio ataonekana, na mtetezi wake atajikita kwenye hilo zaidi, na si vinginevyo. Kitakachomtetea hapo, zaidi ni uwezo wake wa kufanya kazi ambao aliuonyesha wakati anafanya kazi na yule mtetezi wake.

Mara nyingi, walioandaliwa kazi, majina yao yanasomeka na kusambaa haraka sana. Kwa kawaida, watu walio makazini ambao wameandaliwa, huwa sio watendaji wazuri wa kazi. Wao wanajua na wana uhakika, yuko mtu juu wa kuwalinda, hivyo hawahitaji wala hawaoni sababu ya kuhangaika. Mathalani, hata wakikosea, huwa hawana wasiwasi kwani wanajua kuwa makosa yao yatachukuliwa kiwepesi wepesi tu, kwa vile wana watetezi wazito huko juu. Maisha ndivyo yalivyo.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Kushindwa Ni Sehemu Ya Maisha

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Wengi wetu katika maisha, kuna mambo ambayo huwa tunapanga kuyafanya. Unaweza kupanga kwa muda wa dakika tano au kumi, inategemea, haijalishi. Kwa mfano, mtu akienda shule mpaka chuo, kwa kawaida anategemea kuwa akimaliza masomo yake atakuwa mtu mkubwa na mwenye nafasi katika jamii yake.

Mara nyingi, kile unachochagua na kupanga hakiendani na uhalisia wa maisha, yaani maisha ya yale yanayotokea. Unaweza kujikuta, ile nafasi uliyokuwa unaifikiria kuwa utaipata, inakuwa ni ndoto tu. Mwishowe unajikuta unaishia kufanya shughuli ambazo hukuzitegemea. Hapo ndipo unaanza kupata changamoto katika maisha yako. 

Kama ni mfanyakazi, unategemea kupanda cheo, lakini unakuta hupandi kwa wakati. Hali kadhalika, kama ni mfanya biashara, unakuta biashara zako haziendi vile ambavyo ungependa iwe.

Kwa ujumla, kufeli ama kushindwa kufikia malengo yako ni moja ya changamoto katika maisha ya mwanadamu. Matatizo na changamoto haziepukiki katika maisha. Ili mwanadamu aweze kusonga mbele ni lazima azipitie, hakuna jinsi. 

Wakati huo unatakiwa kuwa makini sana maana unaweza kuingia kwenye maamuzi mabaya. Changamoto ziwe mwalimu wako, zikufanye ujifunze yale unayotakiwa kufanya baada ya kuzipitia. Changamoto ziwe ni fursa kwako kukuwezesha kufanya maamuzi ya kubadili ama kutafuta njia nyingine ya kuendeleza biashara yako. Unaposhindwa kwa hili ujue kuna mahala pako pa kujjishindia. Kumbuka, changamoto ni mtaji. Wakati unapitia eneo hilo, eneo la changamoto, uwe na furaha kwani mwanga utakuwepo mbele yako. Mafanikio huwa yako mbele yako.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Akumulikaye Mchana Usiku Hukuchoma

Caroline Swai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Maadam tunaishi hapa duniani, tunakutana na marafiki wazuri, wabaya, wanafki, wambea na wengine wengi tu. Kwa mfano, rafiki yako unayemwamini sana anaweza kukutania, kukutishia au kukusema vibaya hadharani, yaani waziwazi, lakini kwa kuwa ni rafiki yako mmeshibana, unaona ni utani au kawaida tu, na unaweza ukamchukulia poa.

Continue reading “Akumulikaye Mchana Usiku Hukuchoma”
%d bloggers like this: